|
Menu
Passport Procedures
Processing Zones
Answers to FAQs
Passport Forms
Immigration Update
|
Utaratibu wa utoaji wa Pasipoti Mpya
Ufuatao ni utaratibu wa kushughulikia zoezi
hilo katika nchi za uwakilishi wetu*:
A.
KUNUNUA FOMU
- Mwombaji anaweza kuja Ubalozini na pasipoti
aliyonayo ili kununua fomu au atume dola 10,- (malipo
ya fomu kwa rejista) pamoja na kopi mbili za
pasipoti aliyonayo kurasa za 1 hadi 5 na ukurasa
wa mwisho wenye DN. Namba. Aidha, alete bahasha
yenye anuani yake iliyobandikwa stampu za
rejista ili apelekewe fomu.
- Malipo yakipokelewa, mwombaji atapewa fomu
au atapelekewa fomu husika ambayo ataijaza
BILA kuweka sahihi yake katika sehemu ya
sahihi, ukurasa wa kwanza. Mwombaji ataileta
fomu yake, `photocopy' ya fomu iliyojazwa na
picha tano (5) za pasipoti saizi ya 4 x 4.5 cm
zenye `background' ya rangi ya `sky blue' au
rangi ya maji ya bahari. Picha hizo lazima ziwe
za karibuni sana zinazoonyesha masikio yote
mawili.
*FOMU IJAZWE KWA HERUFI KUBWA!
- a) Wakati wa kujaza fomu `Section 2' tarehe,
mwezi na mwaka wa kuzaliwa wazazi ni LAZIMA.
Hata wazazi waliofariki.
b) Kama kuna sababu ya kubadilisha jina
lazima hati husika za sababu ya kubadili jina
ziletwe - k.m. cheti cha ndoa.
c) Kama pasipoti imepotea LAZIMA ripoti ya
polisi na `affidavit' (hati ya kiapo) mbele ya
mwanasheria zitumwe pamoja na fomu.
Wale watakaopenda kuja Ubalozini kununua fomu
na kurudisha fomu wazingatie utaratibu
ulioelezwa (1 - 3).
d) Acha au usijaze kipengele cha sita (6)
katika fomu kwa kuzingatia Maelezo Muhimu kwenye
kipengele cha pili (2) - waliotajwa hawapatikani
nje ya Tanzania.
e) Kila fomu ina namba moja haitumiki kwa
watu wawili. Mwombaji asithubutu kutoa nakala
(photocopy) ili itumike kwa mwombaji mwingine.
- Inatahadharishwa kuwa fomu za uombaji
pasipoti zilizokosewa au kufutwafutwa
hazitakubalika itabidi mwombaji anunue fomu
nyingine. Ni vema kabla ya kujaza fomu mwombaji
atoe nakala (photocopy) ya fomu aijaze kwanza
kila kipengele ili baadaye anakili katika fomu
aliyopelekewa kuepuka makosa, kufutwafutwa na
kununua fomu nyingine.
B. ALAMA ZA VIDOLE NA TAHADHARI
- Katika utoaji wa pasipoti mpya lazima
mwombaji achukuliwe alama za vidole (`finger
prints') na kuweka sahihi kwa mkono wake
mwenyewe mbele ya afisa mhusika. Hivyo, tarehe
ya kuchukuliwa alama za vidole; mwombaji
atajulishwa kwa simu au e-mail.
- Mwombaji LAZIMA aje UBALOZINI ili kutia
sahihi fomu na kuchukuliwa alama za vidole.
Mwombaji atatakiwa alipe dola 40,- malipo ya
pasipoti mpya.
- Maombi yatashughulikiwa ipasavyo na
kupelekwa haraka Makao Makuu ya Uhamiaji Dar es
Salaam katika mfuko maalum wa Kidiplomasia.
- Pasipoti mpya zitatolewa Makao Makuu ya
Uhamiaji, Dar es Salaam na zitaletwa Ubalozini
kwa mfuko maalum.
- Ubalozi utatuma pasipoti mpya kwa mwombaji
kwa kutumia bahasha iliyoandikwa anuani na
mwombaji na kuwekwa stampu za rejista. Pasipoti
ya zamani itabidi iwe ´cancelled' ili nayo
irudishwe kwa Mwombaji katika bahasha moja na
pasipoti mpya. Hivyo, mawasiliano na Ubalozi ni
muhimu kwani pasipoti mpya haitatolewa kabla ya
zamani kuwa `cancelled'. Watakaotaka kufuata
pasipoti zao wenyewe ni ruksa.
- Utaratibu mzima wa kushughulikia unatazamiwa
kuchukua wiki sita (6) au zaidi. Jumla ya
gharama ni $50, yaani $ 10 za fomu na $40 za pasipoti.
*NB:
(i) Pasipoti mpya zitatolewa kubadilisha zile
ambazo zilizotolewa kihalali na zenye kumbukumbu
za utoaji kwa raia wa Tanzania. Siyo kwa wale
wenye uraia wa nchi nyingine walio na pasipoti
mbili. Kisheria nchi yetu hairuhusu `dual
citizenship'; kufanya hivyo ni kinyume cha
sheria. Akigundulika mwombaji mwenye uraia
wa Tanzania na nchi nyingine atachukuliwa hatua
kwa mujibu wa sheria.
(ii) Watoto watapewa pasipoti zao kwa
kuzingatia utaratibu ulioelezwa.
Watoto wa umri usiozidi mwaka mmoja
hawatachukuliwa alama za vidole - wengine zaidi
ya mwaka mmoja lazima wachukuliwe alama za
vidole.
(iii) Watanzania wanaokwenda nyumbani siku za
karibuni wanashauriwa na wanaruhusiwa kuomba
pasipoti mpya wakati wakiwa nyumbani katika
ofisi za uhamiaji Tanzania. Kufanya hivyo
kutawaharakishia kupata pasipoti hizo.
Angalia pia:
|